Tuesday, October 18, 2016

SAIDI FELLA,ANA BIFU NA MKALI WA MUZIKI BARANI AFRICA(DIAMOND PLATNUMZ)? HAYA NDIYO MAJIBU YAKE>>>>>>

SAIDI FELLA( MENEJA YAMOTO BAND,TMK WANAUME FAMILY,DIAMOND PLATNUMZ)
BAADA ya hivi karibuni kudaiwa kuwa ana bifu na msanii wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, bosi wa Yamoto Band, Said Fella, amefunguka kuwa tetesi hizo siyo za kweli na haijawahi kutokea.
Habari kutoka kwa vyanzo mbalimbali zilidai kuwa wawili hao waliingia kwenye bifu baada ya wasanii wa Bendi ya Yamoto anayoisimamia kumlalamikia Diamond ambaye pia ana hisa kwenye bendi hiyo kwamba mkurugenzi wao huyo anawanyonya na kazi zote wanazopiga wao wanamnufaisha yeye tu!

SAIDI FELLA(MKUBWA FELLA) ALISEMA,“Hakuna kitu kama hicho na haijawahi kutokea kabisa, hayo ni maneno tu ya watu na wala mimi na Diamond hatujawahi kuzungumza kitu kama hicho.”
MWANAMUZIKI MASHUHURI BARANI AFRICA,DIAMOND PLATNUMZ...
 
 
 

No comments:

Post a Comment