OLIVE KIARIE,AKILIA KWA FURAHA
Hii ni mara ya kwanza kwa taji hilo kwenda nje ya Tanzania ikiwa ni msimu wa tano toka mashindano haya yaanze mwaka 2009. Olive anakua msichana wa pili kujishindia taji hilo baada ya Bernick Kimiro aliyeshinda mwaka 2012.Shindano la Maisha Plus lilijumuisha washiriki 30 kutoka nchi tano za Burundi, Kenya, Rwanda, Tanzania na Uganda ambapo washiriki 16 tu ndio waliofanikiwa kuingia fainali.Washiriki Aloyce Sambuta, Irene Ishengoma, Alex Essau, Ngenda Pilly, Nibigira Baswari, Grace Pemba, Denaice Machocho, Umubyeyi Solange, Assimwe Marvin, Salmin Omary, Rukia Athuman, Mike Curtywer, Yasinta Mrisho, Karekezi Jean na Namita Cherrie walifanikiwa kuingia fainali ambazo zilirushwa juzi usiku na kituo cha televisheni cha Azam Two.Katika hatua nyingine washiriki wanne walipewa tuzo. Aloyce Sambuta alipata tuzo ya Rais bora na kupewa jumla ya Tshs.Laki nne, Ngenda Pili alipata tuzo ya mshiriki mwenye heshima kubwa, Mike Cutywer alipaza tuzo ya mshiriki mdogo wa kiume wakati Namita Cherrie alipata tuzo ya mshiriki mdogo wa kike.Wasanii Ommy Dimpoz na Joh Makini walitoa burudani wakati wa fainali hizo.
MGENI MUALIKWA,AKIMTANGAZA MSHINDI
No comments:
Post a Comment