Wednesday, October 5, 2016

MAPENZI HISIA: HIZI NI SABABU CHACHE ZA KITAFITI ZA KWA NINI BAADHI YA WANAWAKE HULIA MARA BAADA YA KUFANYA MAPENZI(SEX)>>>>>

Kulia baada ya kushiriki ngono au kufanya mapenzi ni kawaida na hushuhudiwa sana kwa wanawake, ijapokuwa imesemekana kuwa hata wanaume hulia pia.

Kulingana na wataalam mbalimbali, kuna sababu kadhaa ambazo humfanya mwanamke kulia au kujawa na huzuni baada ya kushiriki ngono, na mojawapo ya sababu hizo ni homoni ambazo mwili wa binadamu hutoa wakati huo.

Umewahi kushiriki mapenzi na kugundua kuwa mpenzi wako amelia tu, baada ya kipindi kirefu cha kufurahishana?

----Kulingana na wanasayansi, ni kawaida juu ya situation hiyo.

Utafiti mwingine umeonyesha kuwa, kati ya asilimia 7.7 na asilimia 32.9 ya wanawake wamewahi kulia baada ya kushiriki mapenzi.

---Mara kwa mara, wanaume hulia pia.


Mtaalam mmoja ameielezea hali hiyo kama 'hali ambayo mwanamke hushindwa kujidhibiti na kulia bila sababu, hasa baada ya kupandwa na raha ya kujamiiana, au kufika katika upeo wa raha ya kujamiiana (orgasm.)


Umewahi kudhani kuwa 'ustadi' katika kufanya tendo hili takatifu  ndio uliosababisha kulia kwa mwanamke baada ya kushiriki ngono? Pole sana!

Hata hivyo, mtaalam mwingine amesema kuwa ukweli wa mambo na mawazo yanayokuja punde baada ya kushiriki ngono kama woga, huweza kumfanya mwanamke kulia, ijapokuwa amesisitiza kuwa kulia kwa mwanamke baada ya kushiriki mapenzi ni kawaida!


#MACHAS OFFICIAL SITE

No comments:

Post a Comment