kitendo cha Kuwasili kwa vijana hao katika kijiji hicho ambacho hakijulikani kilipo, kilikuwa kikirushwa live kupitia kituo cha runinga cha Azam Two. Wakiwa na mabegi yao mkononi, washiriki hao walipokelewa na mwanzilishi wa kipindi hicho,ndugu Masoud Kipanya huku wakiwa wamefunikiwa vitambaa vyeusi machoni.
Mshindi wa shindano hilo atajinyakulia kitita cha shilingi milioni 30. Washiriki wote watapewa shilingi 7,000 kwa wiki ili kujikimu wakiwa kwenye kijiji hicho kilichopo katikati ya msitu. Lengo la kupewa shilingi 1,000 kila siku ni kuwafunza maisha ya waafrika wengi ambao huishi chini ya dola moja kwa siku.
Hakuna nyumba kwenye kijiji hicho na hivyo watatakiwa kujenga nyumba zao wenyewe za kuishi.
Tazama picha Zaidi
No comments:
Post a Comment