Saturday, August 6, 2016

VIDEO: MASTAA TAKRIBANI 40 WENYE USHAWISHI MKUBWA MTANDAONI KUNUFAIKA.......INGIA UONE HAPA

MSANII WA KIMATAIFA KUTOKA TANZANIA DIAMOND PLATNUMZ,NI MOJA KATI YA MASTAA HAO ZAIDI YA 40 WENYE USHAWISHI MKUBWA MITANDAONI...
 
MASTAA HAO WAKIPATA PICHA YAO KWA UJUMLA....
Kwa muda mrefu sasa wasanii wenye followers wengi kwenye mitandao ya kijamii nchini wamekuwa wakiingiza fedha kutoka kwa watu na makampuni yanayotaka kutangaza biashara kwenye akaunti zao lakini hakukuwa na utaratibu rasmi na bei zilizopangwa kiutaalamu. Na sasa kampuni ya matangazo nchini, Aggrey & Clifford imezindua app maalum kwaajili ya kusimamia matangazo ya kwenye mitandao ya kijamii ikihusisha mastaa wenye ushawishi zaidi Tanzania. App hiyo iitwayo Binary, imezinduliwa juzi august 1 2016 kwenye hoteli ya Hyatt Regency na kuhudhuriwa na mastaa takriban 40 wa kwanza waliosanishwa kwenye app hiyo.
Akiongea kwenye uzinduzi huo, Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni ya Aggrey & Clifford, Rashid Tenga alisema kuwa waliamua kutengeneza application ya simu itakayoweza kupandisha matangazo kwenye akaunti za mitandao ya kijamii za mastaa waliosaini mkataba bila wao kuhangaika kuyaweka.Tofauti na njia ya kawaida ya kuweka matangazo hayo, app ya Binary inawawezesha kujua ni muda upi watu wanasoma zaidi matangazo (prime time) na hivyo kuwekwa katika muda muafaka. Pia walitengeneza gharama husika (rate card) kwa kuzingatia wingi wa followers alionao staa husika. Alidai kuwa hadi sasa wamesaini mastaa 40 wanaowapa uhakika wa kuwafikia watu zaidi ya milioni 30.
“Hiyo ni zaidi ya jinsi gazeti linavyoweza kukupa, TV yoyote, na redio yoyote,” alisisitiza Tenga.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara wa Binary ,kampuni ya Aggrey & Clifford, Eni Kihedu alisema kuwa kwa utafiti waliofanya, matangazo kwa njia ya mitandao ya kijamii yanafikia watu wengi kwa asilimia 100 zaidi, ukilinganaisha na kuweka tangazo kupitia magazeti.
“Ukicompare digital media houses ambayo ni kutangaza kupitia social media houses ukiweka post zako 10 kwa kila mtu, kwa mwezi kama wanavyofanya kwenye magazeti tangazo linaonekana kuliko kwenye traditional print media na hiyo ni the same kwa radio na TV, with different percentages for radio and TV ingawaje bado ni faida kubwa sana kuliko kutangaza kupitia traditional media,” alisema Ms Kihedu.Mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo, Prof Elisante Ole Gabriel ambaye aliisifia kampuni ya Aggrey & Clifford kwa kuanzisha utaratibu huo utakaokuwa na manufaa makubwa kiuchumi kwa mastaa wa Tanzania.

Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo, Prof Elisante Ole Gabriel akiwa na CEO wa Aggrey & Clifford, Rashid Tenga

ANGALIA VIDEO HII KUJUA UNDANI WA APP YA BINARY ITAKAVYOWANUFAISHA MASTAA HAO....
 
#MACHAS OFFICIAL SITE

No comments:

Post a Comment