Monday, August 15, 2016

SOKA,DUNIANI:- LIONEL MESSI AKATISHA RASMI KAULI YAKE YA KUTOICHEZEA TIMU YAKE YA TAIFA ARGENTINA



Mshambuliaji wa Argentina (na Barcelona) Lionel Messi ambaye mwezi Juni alitangaza kwamba hatoichezea tena timu ya taifa ya Argentina, amebadili mawazo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kupitia gazeti la Argentina liitwalo La Nacion, Messi amekubali kuitikia wito wa kocha mpya wa Argentina Edgardo Bauza na amethibitisha kwamba atakuwepo kuichezea tena Argentina endapo ataombwa kufanya hivyo.
Messi amenukuliwa akisema,”nimeangalia na kugundua kwamba soka la Argentina lina matatizo ya kutosha na mimi sitaki kuwa sehemu ya matatizo hayo. Siku zote nimekuwa upande wa kutatua matatizo kadiri ninavyoweza”
Kwa maana hiyo bila shaka Lionel Messi atakuwepo kuichezea Argentina katika mchezo wa kufuzu kwenda Kombe La Dunia dhidi ya Uruguay utakaofanyika mwanzoni mwa mwezi Septemba.
Messi ambaye anaaminika kuwa mchezaji bora kushinda wote duniani hivi sasa sambamba na Christiano Ronaldo wa Ureno na Real Madrid, ameshashinda tuzo ya FIFA ya Mchezaji Bora wa Dunia (Ballon d’Or) mara tano.

#MACHAS OFFICIAL SITE

No comments:

Post a Comment