FORMER PRIME MINISTER TANZANIA HON.EDWARD NGOYAI LOWASSA....
Msafara wa aliyekuwa mgombea wa Urais kupitia Chadema,pia waziri mkuu mstaafu Edward Lowassa umekwama kwenda Mikoa ya Rukwa na Katavi baada ya polisi kuuzuia kwa hofu kwamba unaweza kuingilia ziara ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anayetembelea mikoa hiyo.
Lowassa ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema alianzia ziara yake mkoani hapa tangu Agosti 21 na juzi alifanya vikao vya ndani katika majimbo yanayoshikiliwa na wabunge wa chama chake mkoani Songwe wakati leo asubuhi alitarajiwa kwenda Katavi na Rukwa.
Katika Mikoa ya Rukwa na Katavi alitarajiwa kufanya mikutano ya ndani Majimbo ya Nkasi Kaskazini na Kusini na Sumbawanga.
Katibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini wanayoiita ‘Kanda ya Nyasa’, Frank Mwaisumbe alisema kwamba polisi walimpigia simu Lowassa juzi saa 1.00 jioni akiwa Tunduma wakimtaka aahirishe ziara yake Mkoa wa Rukwa.
Kamanda wa polisi Mkoa wa Rukwa, Gorge Kyando alipoulizwa kwa njia ya simu alisema waliwashauri viongozi wa Chadema wapange siku nyingine ya ziara kwa sababu mkoa ulikuwa na ugeni mkubwa.

#machas OFFICIAL SITE
No comments:
Post a Comment