Saturday, August 20, 2016

NAMNA PROF SAFARI WA CHADEMA NA KATIBU MKUU BAVICHA WALIVYOPATA AJALI APO JANA TAREHE 19 AUG 2016 SINGIDA

Singida
Jana, Agosti 19, 2016, Makam Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Taifa, Prof. Abdallah Saffari Katibu Mkuu wa Baraza la Vijana la Chadema (BAVICHA) Julius Mwita na dereva wao bwana Abas, jana walipata ajali mbaya ya gari katika maeneo ya Kitalaka, Itigi mkoani Singida.
Akiwasiliana na baadhi ya waandishi wa habari  kwa njia ya simu, Afisa Habari wa Chadema, Tumaini Makene  amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kueleza kuwa wote walitoka wazima hakuna aliyefariki japo dereva abasi ndiye aliyeumia kwenye paji la uso na kupelekwa hospitali kwenda kutibiwa. Abas alishonwa nyuzi na baadaye safari yao iliendelea.
 
#MACHAS OFFICIAL SITE

No comments:

Post a Comment