Saturday, August 27, 2016

CHRISTIANO RONALDO,MCHEZAJI BORA BARA LA ULAYA 2015/2016

CRISTIANO RONALDO,MCHEZAJI KANDANDA MAHIRI DUNIANI....
Mshambuliaji wa Real Madrid na Portugal, Christiano Ronaldo, amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Bara La Ulaya kwa mwaka 2015/2016.
Ronaldo ambaye ndani ya msimu huu ameshinda Kombe La Klabu Bingwa Ulaya (UEFA Champions League) akiwa na Real Madrid na Kombe La Mataifa Ulaya (Euro 2016) ametangazwa mshindi katika sherehe zilizofanyikia Monaco.
Ronaldo amewashinda mchezaji mwenzake wa Real Madrid, Gareth Bale na Antoine Griezman wa Atletico Madrid , Ufaransa.
Mshindi wa Mchezaji Bora wa Ulaya hupatikana kwa kura za waandishi wa habari wa soka kutoka katika nchi 55 zinazounda Shirikisho La Soka Ulaya (UEFA).

HIVI NDIVYO ALIVYOTANGAZWA KUWA MSHINDI:-

#MACHAS OFFICIAL SITE

No comments:

Post a Comment