Tuesday, May 3, 2016

NYOTA WA FILAMU NCHINI MAREKANI KUISAIDIA FAMILIA YA MWANAMUZIKI MAREHEMU PRINCE NELSON ALIEFARIKI HIVI KARIBUNI

NEW YORK, MAREKANI

FAMILIA ya marehemu, Prince Nelson, sasa itakuwa sehemu salama baada ya nyota wa filamu nchini Marekani, George Lopez, kujitolea kuisaidia familia hiyo kifedha.
Inadaiwa kwamba wakati wa uhai wake, Prince alikuwa ni mtu wa kupenda kuisaidia familia yake kama vile mke na mtoto wake, lakini kulikuwa na ndugu zake walikuwa wakimtegemea katika kuongoza maisha yao hivyo familia hiyo itaendelea kufurahia maisha hayo kutoka kwa Lopezi.
TMZ imeweka wazi kwamba, Lopez tayari ameanza kutoa dola 20,000 kwa ajili ya familia ambayo ilizungukwa na marehemu Prince.
Hata hivyo, Lopez amesema ataendelea kufanya hivyo kila wakati kwa ajili ya familia hiyo ili iendelee kuishi katika maisha yao ya awali na kufurahia maisha yao.

No comments:

Post a Comment