Saturday, March 19, 2016

Dyna Nyange afunguka jinsi anavyomzimia Idriss,ila kasema hapendi kutoka na mastaa..


 Msanii wa bongo fleva dyna Nyange amefunguka na kusema kuwa amekuwa akimzimia Idriss ambaye ni mshindi wa
shindano la Big Brother Africa na kwa sasa yuko kwenye mahusiano na Wema sepetu.

Dyna amesema kuwa vitu vinavyomvumtia kutoka kwa staa huyo ni pamoja na mwonekano na ucheshi.“Nampenda Idriss kwa sababu kwa mwonekano wa karibu ni mtu ambaye anajitambua,anajielewa,gentleman..zile comedy na...jua kabisa ntakuwa nacheka tu ndani,hamna kununa” alifunguka mwanadada huyo
Hata hivyo Dyna Nyange ameongeza kuwa hapendi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mastaa kwa sababu wengi
wanakuwa pasua kichwa na yeye ni mwanamke mwenye wivu.”Sijawahi kufikiria ku date na wasanii kwa sababu
nawaogopa,ni pasua kichwa..mimi nina wivu sana mazingira ambayo tuko nayo nadhani nitakonda mara mia” alimaliza staa huyo.

Source: Clouds
 

No comments:

Post a Comment