WATU watano wamefariki dunia huku wengine nane
wakijeruhiwa, katika ajali iliyoyahusisha magari manne, mawili yakiwa katika
msafara wa Kamati ya Bunge Utawala na TAMISEMI maeneo ya Kerege, Bagamoyo
mkoani Pwani.
Waliofariki katika ajali ni Hilda Msele (59), Mkuu
wa Idara ya Mipango ya Uchumi, Makame Ally (40), Dereva wa Tasaf, Khalid Hassan
(40), Tunsime Duncan, Mwanasheria wa Wilaya na Ludovick Palangya, Mchumi.
Majeruhi waliolazwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili ni
Ibrahim Matovu, Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Bagamoyo, Juliana Msaghaa,
Mhandisi wa Maji wilaya, Dorothy Njetile, Mratibu wa Tasaf, George Mashauri,
Mweka Hazina wa Wilaya, Amadeus Mbuta, Mshauri wa Tasaf, Julius Mwanganda, Mkuu
wa Idara ya Maendeleo ya Jamii, Tauliza Halidi, Mwananchi na Amari Mohamed,
Mwananchi.
Aliyepelekwa katika Hospitali ya Wilaya ya Bagamoyo na
kuruhusiwa ni George Mbilinyi ambaye ni Afisa Utumishi na Utawala wa Wilaya.
Ajali hiyo iliyohusisha lori la mchanga,
gari dogo yote yakitokea Bagamoyo kuja Dar es Salaam, na magari mawili
yaliyokuwa kwenye msafara wa Kamati hiyo, yaliyokuwa yanaenda Bagamoyo kwa
shughuli zake za kibunge.
Magari yaliyokuwa katika msafara wa kamati hiyo, ni gari la
Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf) na gari la Mkurugenzi wa Wilaya ya Bagamoyo
ambayo yaligongwa na lori hilo la mchanga na kusababisha vifo vya watu hao na
kuwajeruhi wengine kadhaa.
Ajali hiyo ilitokea baada ya gari dogo lililokuwa linatokea
Bagamoyo kupunguza mwendo ghafla na kusababishwa lori lililokuwa nyuma yake
kuligonga na kuhama upande wa pili na kuyagonga magari mawili yaliyokuwa katika
msafara wa kamati ya Bunge.
TASWIRA YA HALI HALISI-BY MACHAS OFFICIAL
No comments:
Post a Comment