Tuesday, April 25, 2017

WORLD PLUG: UPASUAJI WA KUBADILI JINSIA(KIUME-KIKE) YA JENNER KUA MWANAMKE WAKAMILIKA>>>>

Kweli Ukiyastaajabu ya Mussa, utaona ya Firauni. Caitlyn Jenner ni mwanamke ambaye awali alifahamika kama Bruce Jenner, mshindi wa mbio za Olimpiki miaka ya 1970 na baba wa kambo wa familia maarufu duniani ya Kardashians, wakiwemo Kim, Khloe, Kylie na Kendall. Bruce kwa kutoridhika na jinsia yake, amechukua hatua ya kufanya upasuaji wa kubadilisha jinsia. Hatua ambayo ilianza takriban miaka miwili iliyopita...
BRUCE JENNER(KIPINDI AKIWA MWANAMUME)
Upasuaji huo umekamilika huku Bruce na sasa Caitlyn kwa kubadili jinsia yake ya kiume na kuweka ile ya kike pamoja na kuweka maziwa na ‘hormones’ za kike mwilini mwake
“Ninawaambia kwa sababu nimeamua kuwa mkweli” alieleza Caitlyn,”Mlikuwa mnataka kujua kama nitaweka jinsia hii ama la. Sasa nimeamua kuweka wazi. Hii ni mara yangu ya mwanzo na mwisho kuzungumzia mabadiliko ambayo tayari nimeyafanya.” Caitlyn alimalizia kwa kiusema, “nNisingependa kuyazungumzia tena.”
Kwa mujibu wa chanzo cha karibu na Caityln, mwana mama huyo kwa sasa anategemea kufanya photoshoot ambayo itamuonyesha katika uhalisia wa jinsi alivyo sasa.
CAITLYN JENNER PREVIOUS BRUCE JENNER
Kutoka katika chanzo cha Familia ya Kardashian, akiwemo Kris Jenner, aliyekua mke wa Bruce kwa miaka 25 kabla ya kuamua kubadili jinsia yake, anatamani jambo hili, ambalo hawakutegemea yapitekwa sababu sio jambo jema kwao....
 
WATCH THE VIDEO>>>>

No comments:

Post a Comment