Thursday, November 3, 2016

TAZAMA VIDEO YA UNDANI,IKIELEZEA UNYAMA ALIOFANYIWA MSICHANA,AITWAE JULIANA ISAWAFO,AMBAE AMEKUTWA AMEFARIKI KWENYE SHAMBA MOJA LA MPUNGA,MAKUMIRA UNIVERSITY JIJINI ARUSHA>>>>

JULIANA ISAWAFO,ENZI ZA UHAI WAKE
Mapema juzi zimesambaa Picha kwenye Mitandao ya kijamii zikimuonyesha Msichana anayefahamika kwa jina la JULIANA ISAWAFO Ambaye Amebakwa hadi Kufa na Kutupwa Nje ya eneo la Chuo Kikuu cha Tumaini (Makumira Arusha).

Mmoja wa Viongozi wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo hicho ambapo amethibitisha kwamba ni kweli Ameokotwa Msichana huyo Majira ya Saa tano asubuhi ya jana tarehe 03 November 2016, akiwa Amekufa na mwili wake Kutelekezwa kwenye Shamba la Mpunga hatua chache nje ya Eneo la Chuo.

Hata hivyo Amethibitisha kwamba Msichana huyo ni Mwanafamilia wa Chuo cha Makumira ila sio Mwanafunzi rasmi kama watu wanavyodai.

Anasema Msichana huyo alikuwa akiishi ndani ya eneo la Chuo kwa Mzungu mmoja ambaye ni mmoja wa waalimu wa Sanaa Chuoni hapo.

Hata hivyo hakusita kuweka wazi kwamba Wanasikitika sana Kwa Tukio hilo kwani Msichana huyo alikuwa kama Dancer wa Matamasha ya Chuo cha Makumira.

  Sikiliza Hapa chini:
imesikitishwa na unyama aliotendewa mschana huyo,hivyo kuiomba serikali,ichunguze kwa makini kujua ni akina nani wanahusika,ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa na mamlaka zinazohusika
 
"pumzika kwa Amani,mpendwa"
 

No comments:

Post a Comment