Monday, September 5, 2016

MWANAMUZIKI JUMA "JUX" AMESEMA KUWA SHOW YA "FIESTA"IMEMFANYA ATAMBUE KWAMBA KUMBE ANAFANBASE KUBWA KULIKO ALIVYOFIKIRIA HAPO AWALI >>>>

JUX,MWANAMUZIKI MAHIRI WA R&B KUTOKA TANZANIA
Kwa miaka mingi Jux amekuwa akiachia muziki tu AMBAO  unafanya vizuri na kushindwa kuzunguka kwenye mikoa mingi nchini kutumbuiza kutokana na kubanwa na masomo, lakini kupitia Fiesta, muimbaji huyo amesema amegundua kuwa ana mashabiki wengi kuliko alivyotarajia.
-------
Ameiambia chaneli moja ya burudani kuwa, kote ambako show hiyo imepita, amekuwa akiwaacha mashabiki wakitaka zaidi vitu kutoka kwake.
“Nimegundua kwamba nina fanbase kubwa sana Tanzania hata sehemu zingine nilizokuwa nahisi labda bado,sifahamiki nimejua baada ya Fiesta,” amesema Jux.
“Nimegundua kwamba muziki unasafiri sana, watu wamefurahi hata mimi nimefurahi kwasababu mikoa mingi nilikuwa sijawahi kwenda kama Shinyanga, Muleba , Singida pia sijawahi kwenda naenda sasa hivi,” ameongeza.
Jux anayefanya vizuri na wimbo wake ‘Wivu’ ameongeza kuwa ameweza pia kugundua jinsi muziki wa Tanzania ulivyokuwa na ukubwa wa kushangaza.

#MACHAS OFFICIAL SITE

No comments:

Post a Comment