Monday, July 4, 2016

NYOTA WA MICHANO BONGO MR BLUE, KABAYSER AMESEMA WANAODHANI AMEFULIA WAMEULA WA CHUYA.

MKALI WA MICHANO BONGO MR BLUE
 
 
Kama unadhani Mr Blue ni miongoni mwa wale wasanii wanaoishia kuwa maarufu tu lakini maisha yao yakiwa bado ‘hayaendani na ustaa’ upo wrong.

Rapper huyo amesema kuwa hadi sasa ana nyumba tatu na zote zimetokana na muziki.

“Moja naishi, mbili zingine ndio ambazo najaribu kumaliziamalizia,” Blue alikiambia kipindi cha The Playlist cha Times FM Jumamosi iliyopita.

Hata hivyo Blue anasema kama angekuwa na akili hizo za maisha tangu miaka ya nyuma kwa sasa angekuwa na mali nyingi za kutisha lakini ujana na matumizi ya vilevi vilimponza.
 
"MACHAS OFFICIAL SITE"

No comments:

Post a Comment