Friday, May 6, 2016

STAA WA MUZIKI WA POP DUNIANI JANET JACKSON ANATARAJIA KUPATA MTOTO WA KWANZA HUKU YEYE MWENYEWE AKIWA NA UMRI WA MIAKA 50

NEW YORK, MAREKANI

NYOTA wa muziki, Janet Jackson, anadaiwa kuwa na ujauzito wa mtoto wake wa kwanza kama atajifungua salama.
Mrembo huyo anatarajia kufikisha miaka 50 baada ya wiki mbili.
Aprili mwaka huu aliweka wazi kwamba hana mpango wa kufanya muziki kwa sasa kwa kuwa ana lengo la kutulia na mume wake kwa ajili ya kupanga familia, hivyo atachelewa kurudi katika muziki.
Mapumziko hayo yanadaiwa kuzaa matunda ambapo inaonesha wazi kwamba ana ujauzito hivyo anatarajia kupata mtoto wake wa kwanza.
Hata hivyo, msanii huyo ameweka wazi jambo hilo kupitia wimbo wake mpya ambao unajulikana kwa jina la ‘Dammn Baby’ tangu 2008 msanii huyo aliweka wazi kutaka mtoto hivyo ndoto zake zinaweza kuwa zimetimia.


#MACHAS OFFICIAL SITE...

No comments:

Post a Comment