Thursday, April 7, 2016

Dada wa Mh Tundu Lissu, Christina Lissu afariki dunia mchana wa leo

MAREHEMU CHRISTINA LISSU MUGHWAI,ENZI ZA UHAI WAKE.
 
Dada wa Mbunge wa Singida Mashariki, Mh Tundu Lissu na aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum Mh. Christina Lissu Mughwai amefariki dunia muda mfupi uliopita katika hospitali ya Aga Khan Dar. 

Marehemu alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa cancer tangu mwaka jana. Taarifa zaidi kuhusiana na msiba huu tutaendelea kuwajuza na kuwataarifu.

#MACHAS OFFICIAL SITE..., inapenda kutoa pole kwa familia ya Marehemu Christina Lissu pamoja na kwa Mbunge Mh Tundu Lissu kwa kuondokewa na dada yake. Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi 
Amen

PREPARED AND EDITED BY MACHAS OFFICIAL SITE

No comments:

Post a Comment