Sunday, April 9, 2017

ENTERTAINMENT FLICK: JANET JACKSON AACHANA NA MUMEWE,IKIWA NI MIEZI KADHAA TANGU MWANAMAMA HUYU,APATE MTOTO AKIWA NA UMRI WA MIAKA 50>>>>

Miezi michache tu baada ya kupata mtoto wake wa kwanza akiwa na umri wa miaka 50, Janet Jackson ameachana na mume wake bilionea Wissam Al Mana.
Japo vyanzo vimesema wameachana kwa kukubaliana na kwamba watashirikiana kumlea mtoto wao wa kiume, vingine vinasema hawakuwa na maelewano kwa muda.
“Aliona [Wissam] amekuwa muamrishaji sana pindi cha ujauzito wake [Janet] na alikuwa ameshamruhusu kumwamulia muonekano wake na hata jinsi alivyotumbuiza kwenye matamasha,” chanzo kinachofanya kazi na wapenzi hao kilisema.
Janet pia aliacha kufanya video alizokuwa amezoea na hivyo kuhisi anaendelea kupoteza mashabiki wake. Kingine, Jackson alikuwa hapendezwi na kujitenga kwa mume wake, ambaye alikuwa akikutana na ndugu zake kwa nadra sana na pia kutoonesha kuwajali kwenye matatizo.
Walipata mtoto wao, Eissa Al Mana, January 3 2017 ikiwa ni miaka mitano tangu wafunge ndoa

No comments:

Post a Comment