Diamond Platnumz anazidi kufikia malengo aliyojiwekea mwaka huu. Video ya wimbo wake, Marry You aliyomshirikisha Ne-Yo, imeingia kwenye Top 20 za Vevo nchini Marekani. Chati hiyo inahusisha wasanii wapya wa Marekani na wanaotokelezea kwenye soko la muziki marekani.Video hiyo sasa inapigana vikumbo na ngoma za rappers maarufu wakiwemo Designer na Lil Yatchy. “Kwahiyo @vevo ndio wameamua iwe hivyo? Top 20 New Artists Videos in the U.S na #MarryYou imo? Kwanini wanafanya upendeleo?,” ameandika meneja wake, Sallam.Hadi sasa video hiyo ina views milioni 3.7.
No comments:
Post a Comment