Saturday, January 7, 2017

MACHAS OFFICIAL SITE,HUU NI MKUSANYIKO WA PICHA 18,MAZISHI YA ALIYEKUWA MGOMBEA URAIS WA KWANZA MWANAMKE TANZANIA,MAREHEMU DR.ANNA C SENKORO>>>>>

Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Mrisho Kikwete, JANUARY 07 2017 amewaongoza mamia ya waombolezaji katika mazishi ya aliyekuwa mgombea urais wa kwanza mwanamke, DR.Anna C Senkoro aliyefariki Januari 4, 2017 katika Hospitali ya Muhimbili, baada ya kusumbuliwa na maradhi ya moyo kwa muda mrefu.
Mazishi yamefanyika katika Makaburi ya Kinondoni ambapo awali, ilifanyika ibada ya kumuombea marehemu, iliyofanyika katika kanisa la Winners Chapel International, Banana Ukonga DSM, na kuhudhuriwa na wanasiasa mbalimbali, wakiwemo Humphrey Polepole ambaye ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Anne Makinda, spika mstaafu huku Ukawa wakiwakilishwa na Makongoro Mahanga.
Katika Uchaguzi Mkuu wa 2005, marehemu Senkoro alijitokeza kuwania urais, akipambana na Kikwete kwa tiketi ya Chama cha APPT- Maendeleo, hivyo kuweka historia ya kuwa mwanamke wa kwanza Tanzania kuwania nafasi hiyo, tangu kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi.
Marehemu ameacha watoto watatu na wajukuu wawili. Mungu ailaze mahali pema roho ya merehemu. Amina.
 
HIZI NI PICHA ZAIDI ZA TUKIO HILO>>>>
NDUGU HUMPHREY POLEPOLE TOGETHER WITH FORMER SPEAKER PARLIAMENT OF TANZANIA HON.ANNE SEMAMBA MAKINDA
WANAFAMILIA/NDUGU WAKIWA WAMESHIKILIA PICHA YA MPENDWA WAO MAREHEMU SENKORO
Rais Mstaafu, KIKWETE akiweka udongo kwenye kaburi la marehemu Senkoro.
Rais Mstaafu, Kikwete aliongozana na mkewe, Mama Salma Kikwete. Pichani akiweka udongo kwenye kaburi la marehemu Senkoro.
Watoto wa marehemu, wakiongozwa na Joan Jafet (aliyesimama) wakiweka udongo kwenye kaburi la mama yao.
Waombolezaji wakiwa kwenye misa ya mwisho ya kumuombea marehemu, iliyoongozwa na Pastor Samuel Adeyemi (wa kwanza kushoto mwenye biblia)
DR.ANNA CLAUDIA SENKORO,ENZI ZA UHAI WAKE
 
PHOTOS ARRANGED BY
 

No comments:

Post a Comment