JOSE EDUARDO DOS SANTOS
DE PREZEDEE ANGOLA
ANGOLA: Kituo cha radio cha Angola kinasema kwamba, Rais Jose Eduardo dos Santos, ambaye ametawala taifa hilo kwa karibu miongo minne atajiuzulu kabla ya Uchaguzi mkuu, mwaka ujao.
Waziri wa Ulinzi, Joao Lourenco, anatarajiwa kuwa mkuu wa chama kinachotawala cha MPLA. Hii ni kumaanisha kuwa ,yeye atakuwa Rais iwapo chama chake kitashinda uchaguzi mwaka ujao.
Bwana Dos Santos, ambaye ana umri wa miaka 74, wakati mmoja alikuwa kiongozi mchanga zaidi katika Bara la Afrika aliposhinda uchaguzi wa kuwa Rais akiwa na umri wa miaka 34 pekee.
Amewahi kusema kuwa hatashiriki uchaguzi lakini baadaye akabadilisha maoni yake na kusimama tena. Makundi ya kupambana na ufisadi yamemlaumu kwa kuendesha serikali kama biashara ya kibinafsi........
No comments:
Post a Comment