Friday, November 4, 2016

SIKU NITAKAPOLETEWA,MUSWADA WA SHERIA YA HABARI,NITAUSAINI MUDA HUO HUO-JPM>>>

DKT.JOHN POMBE MAGUFULI
RAIS WA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA.
 
story:JULIET MACHA-JOURNALIST MACHA BLOG
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amesema siku akiletewa Muswada wa Sheria ya Vyombo vya Habari atausaini muda huo huo ili uanze kufanya kazi mara moja.
Akizungumza katika mahojiano na waandishi wa habari Ikulu jijini Dar es salaam, Rais Magufuli amesema hawezi kuzungumza lolote kuhusu muswada huo kwa kuwa muswada huo utajadiliwa bungeni na wabunge wote.
“Kuniambia mambo ya bunge ambayo bado sijaletewa, utakuwa unanionea, katika utawala wa bunge,” Magufuli alimjibu mwandishi aliyehoji kuhusu muswada huo. “Tuwaache wabunge watimize wajibu wao. Sasa unaponiambia ukiletwa nikatae nataka nikueleze bila unafiki kuwa,siku utakapoletwa, siku hiyo hiyo nitausaini, ili msubiri kama utakuja wakati mwingine mje muubadilishe, sitaki kufrastuate mambo ya bunge,”
Aliongeza, “Lakini lazima tukubali kwamba hii sheria imechelewa, na unakuta mnazungumza kwa lugha ya wamiliki fulani fulani. Lakini muswada huu sifahamu wabunge watakacho amua lakini nia ni kulinda waandishi wa habari,”
Katika hatua nyingine Rais Magufuli amewataka watanzania kufanya kazi kwa bidii ili wapate kipato kutokana na kazi wanazofanya.
“Tanzania ni tajiri, kinachotakiwa ni namna ya kubalance rasilimali, katika kufanya hilo, mimi nimeamua kubana matumizi serikalini kwa mfano nimedhibiti safari za nje kwa kuanza na mimi mwenyewe, tangu niingie madarakani nimepata mialiko 47 lakini nimekwenda mialiko mitatu tu.” Alisema Rais Magufuli.

ANGALIA VIDEO HII APA CHINI:-
 KAMA ULIIKOSA HOTUBA YOTE,MWANZO HADI MWISHO HII HAPA NIMEKUWEKEA,ENJOY YOURSELF
 
chanzo:VYOMBO VYA HABARI TAREHE 04 NOV 2016
 
BY
 

No comments:

Post a Comment