Kijana mwenye mkia wa sentimita 20 ulioota chini ya uti wa mgongo wake amefanyiwa upasuaji ili kuondoa mkia huo ambao Ulianza kujitokeza katika mgongo wa kijana huyo mwenye miaka 18 baada ya siku yake ya 14 kuzaliwa.
Yeye na familia yake kutoka Nagpur nchini India, walifanya swala hilo kua siri kwa sababu walikuwa na wasiwasi angechokozwa na wenzake, na sasa wameonana na daktari baada ya mkia huo kuendelea kukua na kuota mfupa kwa ndani.
Mkia huo unadaiwa kuwa mrefu kuwahi kutokea kwa mwanadamu licha ya kuwa kesi kama hiyo ni hadimu
Madaktari wanasema kuwa, kijana huyo huenda aliota mkia huo ndani ya tumbo la mamake kutokana na kasoro katika uti wa mgongo, lakini ukaja kuonekana nje baada ya kijana huyo kuwa mkubwa.
#MACHAS OFFICIAL SITE
No comments:
Post a Comment