YOWERI KAGUTA MUSEVENI,RAIS WA UGANDA....
KAMPALA: Watu watatu wanashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Kampala, Uganda kwa tuhuma za kuiba ng’ombe ambao idadi yake haijajulikana vizuri katika shamba la Rais wa nchi hiyo, Yoweri Kaguta Museveni, polisi walisema jana Jumapili.
“Mmoja kati yao anafanya kazi kwenye shamba la rais Museveni.na Walikuwa wakipeleka ng’ombe hao mnadani kuuza,” Mkuu wa Kituo cha Polisi, Doreen Kachwo aliiambia AFP.
“Watuhumiwa hao wamekiri kuiba ng’ombe hao na wamekuwa wakifanya hivyo mara kadhaa hata kabla ya kukamatwa,” aliongeza.
“Baada ya upelelezi kukamilika, watuhumiwa watafikishwa mahakamani ili kujibu tuhuma za wizi zinazowakabili.”
Shamba kubwa la rais Museveni la Kisozi lipo wilayani Gomba, katikati mwa Uganda, ambapo ni takribani kilomita 100 Magharibi mwa Kampala, ambapo kabila la Banyankore linapatikana.
Museveni hupendelea kwenda kule kupumzika hata wakati mwingine kupeleka wageni wake wanaokwenda kumtembelea kutoka nje ya nchi hiyo.
Museveni, ameiongoza Uganda kama rais wa nchi hiyo kwa miongo mitatu sasa tangu mwaka 1985 ambapo mwezi Februari mwaka huu, Museveni alichaguliwa tena kuiongoza nchi hiyo baada ya kumshinda mpinzani wake, Kizza Besigye aliyepinga matokeo ya uchaguzi huo.
#MACHAS OFFICIAL SITE
No comments:
Post a Comment