Saturday, September 10, 2016

MKUU WA WILAYA YA HANDENI MHESHIMIWA GODWIN GONDWE AKAMATA MALORI SABA YAKISAFIRISHA MADINI USIKU!

MKUU WA WILAYA YA HANDENI(TANGA) MHESHIMIWA GODWIN GONDWE.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni mkoani Tanga, Godwin Gondwe amekamata malori saba yakisafirisha madini ya chuma aina  dolomite yanayotumika kutengeneza saruji.
Gondwe amesema kati ya  malori saba walifanikiwa kukamata matano, huku mawili madereva wakiwahi kutoroka. “Malori hayo yalikuwa yanatokea Kata ya Mgambo, yanakochimbwa madini hayo,”
 amesema.
“Tulipokamata magari hayo, kwanza tuliwauliza kama wamelipa kodi na kama wamelipa watuonyeshe stakabadhi,”
Alisema madini yanapo safirishwa hovyo usiku yanakuwa yanasafirishwa kimagendo,hivyo kupoteza mapato,na kadhalika
---Kufuatia hatua hiyo, Gondwe ametangaza kupiga marufuku usafirishaji  madini usiku.
nae Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wilaya za Handeni na Kilindi, Charles Kamuhanda alisema kumekuwa na changamoto ya ulipaji kodi kutoka kwa wafanyabiashara.

No comments:

Post a Comment