Wednesday, September 14, 2016

BARAKA DA PRINCE: KINGEREZA KWANGU BADO NI TATIZO,HIVYO MPANGO WANGU WA SASA NI KUTAFUTA MWALIMU AMBAYE ATANIFUNDISHA KUKICHAPA>>>>>>>>>

BARAKAH DA PRINCE
Msanii wa muziki Barakah Da Prince amekiri kuwa lugha ya Kingereza kwake ni tatizo huku akiweka wazi mpango wa kutafuta mwalimu wa kumfundisha.
Muimbaji huyo ambaye ameachia wimbo WAKE uitwao  ‘Nisamehe’ hivi karibuni akiwa amemshirikisha AliKiba, amesema katika interview yake kubwa iliyopita na kituo kikubwa cha tv MTV kuwa aliomba kutumia lugha ya Kiswahili kwa kuwa ndio lugha ambayo anaweza kuizungumza.
“Niliulizwa kwenye interview ya MTV kama naweza kuongea Kingereza, nilichowajibu naweza ila sio Kingereza kilichonyooka ndio maana nikatumia Kiswahili. Nafurahi kwa kuwa walivutiwa na Kiswahili,” Barakah alikiambia kipindi cha Uhondo cha EFM Jumanne hii.
Pia muimbaji huyo amesema mpenzi wake wa sasa Naj ameshindwa kumfundisha huku akiweka wazi mpango wa kutafuta mwalimu.
“Hanifundishi lugha kwa sababu tuna masihara mengi hivyo nahitaji mtu ambaye atakuwa serious,” alisema Barakah.
#MACHAS OFFICIAL SITE

No comments:

Post a Comment